Mathayo 6 - Usiwe na Wasiwasi

SERMON TOPIC: Mathayo 6 - Usiwe na Wasiwasi

Speaker: Gavin Paynter

Language: SWAHILI

Date: 1 February 2014

Topic Groups:

Sermon synopsis: MATHAYO 6:25-34 “Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi ya mavazi?
Waangalieni ndege wa mwituni: hawapandi, hawavuni, wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, nyinyi si wa thamani kuliko hao?
Ni nani miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza kuuongeza muda wa maisha yake?
“Na kuhusu mavazi, ya nini kuwa na wasiwasi? Tazameni maua ya porini jinsi yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayasokoti.
Lakini nawaambieni, hata Solomoni mwenyewe na fahari zake zote hakupata kuvikwa vizuri kama ua mojawapo.
Ikiwa basi, Mungu hulivika hivyo jani la shambani ambalo leo liko na kesho latupwa motoni, je, si atawafanyia nyinyi zaidi? Enyi watu wenye imani haba!
“Basi, msiwe na wasiwasi: ‘Tutakula nini, tutakunywa nini, tutavaa nini!’
Maana hayo yote yanahangaikiwa na watu wasiomjua Mungu. Baba yenu wa mbinguni anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo vyote.
Bali, shughulikeni kwanza juu ya ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo yote mtapewa kwa ziada.
Basi, msiwe na wasiwasi juu ya kesho; kesho inayo yake. Matatizo ya siku moja yanawatosheni kwa siku hiyo.”

- Download notes (857 KB, 1750 downloads)

- All sermons by Gavin Paynter

- All sermons in SWAHILI




IP:Country:City:Region: